Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma amesema bado mapema kutabiri ni timu gani itatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Baada ya Yanga kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli katika mchezo wake wa kwanza huku wapinzani wao Simba wakipata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, wapo ambao tayari wameipa Simba ubingwa.
Licha kukiri kwamba Simba imejipanga vizuri msimu huu kutokana na usajili wao, Ngoma amesema bado Yanga ina kikosi kinachoweza kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne.
"Kwa sasa timu yetu haipo vizuri kutokana na majeruhi wengi tulionao kama Tambwe (Amissi), Chirwa (Obrey), Beno (Kakolanya) na Mwashiuya (Geofrey), kama hao watakuja kupona wote, nadhani tutakuwa tumekamilika hasa.
"Zamani tulikuwa na tatizo la kiungo mkabaji, lakini tayari limeshatafutiwa ufumbuzi baada ya kusajiliwa Papy Tshishimbi, hivyo wale waliokuwa majeruhi kama wakipona tutakuwa hatushikiki," amesema Ngoma.
Tayari Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya wameanza mazoezi na huenda wakawa tayari kuivaa Njombe Mji kwenye mchezo wa pili wa Yanga, Septemba 06.

ADVERTISE HERE