Kiungo Mohammed Issa 'Banka' anamaliza adhabu yake ya kufungiwa miezi 14 leo na kuanzia kesho yuko huru kuonekana akiwa amevaa uzi wa Yanga
Banka atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili JKT Tanzania keshokutwa Jumapili katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa dimba la Mkwakwani mkoani Tanga
Ujio wa kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, umesubiriwa kwa hamu na Wana Jangwani na hatimae wataweza kushuhudia akiitumikia timu hiyo
Banka amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Yanga tangu mwanzoni mwa Januari mwaka huu
Atatumia jezi namba nane

ADVERTISE HERE