Zahera kuandaa mkakati wa kuimaliza Simba Februari 16

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2019
Zahera kuandaa mkakati wa kuimaliza Simba Februari 16

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ataandaa mkakati wa 'kuimaliza' Simba kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumamosi ya wiki hii

Akizungumza jana baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Zahera alisema hakuwa akifahamu kama mchezo dhidi ya Simba utapigwa Februari 16

"Hata nilikuwa sifahamu kuwa tutacheza na Simba Jumamosi ijayo," alisema Zahera

"Nafahamu Simba wanacheza na Al Ahly wiki hii. Nitakaa na wenzangu usiku huu ili tuone tunajipanga vipi kuelekea mchezo huo"

Aidha akizungumzia ushindi wa Yanga jana, Zahera aliyebadili wachezaji sita wa kikosi kilichoikabili Singida United, alisema wachezaji wake walitimiza wajibu wao kama wanavyofanya siku zote

"Mchezo wa leo haukuwa na tofauti na michezo mingine. Wachezaji wangu wamefanya vile nilivyowaelekeza," alisema

"Labda tofauti ninayoweza kuisema ni kuwa leo waamuzi hawakutukalia goli. Mpira umeingia wavuni mwamuzi akaitika"

Katika michezo miwili dhidi ya Coastal Union na Singida United, Yanga ilifunga mabao lakini yalikataliwa na waamuzi

Inaelezwa Yanga itaelekea mkoani Morogoro kuweka kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’