Kila mchezo kwetu ni fainali - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2019
Kila mchezo kwetu ni fainali - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wanafanya maandalizi kabambe kwa kila mchezo wanaoshuka dimbani akitambua kila mchezo kwao ni kama fainali.

Zahera aliyetua Yanga mwishoni mwa msimu uliopita, amefanya maajabu msimu huu kwa kuiongoza Yanga kushinda michezo 18 kati ya 23 iliyocheza kwenye ligi kuu ya Tanzania licha ya mwanzoni kutopewa nafasi ya kufanya vizuri

Mcongomani huyo amesema baada ya mafanikio hayo timu yake imekuwa ikikamiwa na kila timu wanayokutana nayo.

"Kila mchezo tunaocheza ni kama fainali. Tunatambua ugumu uliopo mbele yetu na tumekuwa tukifanya maandalizi ya kutosha," amesema

Akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi ijayo katika dimba la Taifa, Zahera amesema mchezo huo ni wa kawaidia na maandalizi yake hayana tofauti na michezo mingine.

Amesema tofauti iliyopo ni kwa kuwa mchezo huo unazikutanisha timu zenye upinzani wa jadi ndio maana presha ni kubwa

"Nimebaini hapa Tanzania mchezo wa Simba na Yanga una presha kubwa sana. Viongozi wamekuwa wakiuzungumzia mchezo huo zaidi wakati tukijiandaa na michezo mitatu iliyopita," amesema

"Lakini kwangu mimi mchezo huu ni wa kawaida, tutajiandaa vizuri na lengo letu ni kushinda"

Katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi saa 11 jioni, Yanga itakuwa na deni kwa mashabiki wake kuhakikisha inapata ushindi ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Licha ya Simba kuwa na viporo vingi, wakipoteza mchezo wa Jumamosi huenda ikawa mwanzo wa wao kuliachia taji la ligi kuu.

Yanga inahitaji kufuta uteja kwa Simba kwani katika michezo ya misimu ya hivi karibuni Simba imetawala huku ushindi wa Yanga ukiwa ni matokeo ya sare

Mara ya mwisho Yanga kuifunga Simba kwenye michuano yote ilikuwa msimu wa 2015/16 wakati huo ikinolewa na Hans van Pluijm ambaye sasa ni kocha wa Azam Fc

Katika msimu huo Yanga ilishinda mabao 2-0 katika michezo yote miwili ya ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’