Baada ya kuweka kambi kwa siku nne mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam mapema ili wachezaji wapate muda wa kupumzika
Aidha Yanga itakayokuwa mwenyeji wa mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, itafanya maandalizi ya mwisho leo tayari kwa mchezo huo
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ni muhimu kwa vijana wake kupata mapumziko baada ya kufanya mazoezi makali huko mkoani Morogoro kwa takribani siku nne
Baadae leo, uongozi wa Yanga utazungumza na wanahabari kuweka wazi maandalizi ya kuelekea mchezo huo
Katika hatua nyingine, mashabiki wa Yanga wameaswa wajitokeze kwa wingi katika dimba la Taifa kesho kuiunga mkono timu yao itakapokuwa ikichuana na Simba
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kwa maandalizi waliyofanya, hakuna namna Simba itachomoka kwenye mchezo wa kesho
Viingilio vya mcheoz huo;
