Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga kesho wanashuka katika dimba la Taifa kuwakabili watani zao wa jadi Simba katika mchezo utakaopigwa saa 11 jioni
Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo hivyo mapato yote yatakayopatikana yatachukuliwa na Yanga baada ya kuondoa makato ya wadau wengine
Mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho kwani mbali na kuongeza mapato ya timu, uwepo wao utaongeza hamasa kwa wachezaji
Ukifuatilia kwa umakini kwenye mitandao ya kijamii utabaini Simba haifanyi matangazo ya kuwashawishi mashabiki wake kwenda uwanjani kesho huku baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wakijinasibu kutokwenda uwanjani ili kuinyima Yanga mapato
Wana Yanga watumie hali hii na wafurike uwanjani kwa wingi zaidi ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.
Msimu huu Wana Yanga wameapa kuwa pamoja na timu yao. Wamedhihirisha hilo kupitia michango yao na kesho tukadhihirishe pale uwanja wa Taifa kwa kujitokeza kwa wingi