Yanga imepoteza mchezo wa pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watani zao wa jadi Simba
Simba ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi kwenye kipindi cha kwanza huku Yanga ikitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza
Katika kipindi hicho Yanga ilipoteza nafasi adimu kupitia kwa Makambo
Hata hivyo Yanga ilibadili mbinu kwenye kipindi cha pili na kulishambulia lango la Simba mara kadhaa
Bao pekee la Simba lilifungwa na Meddie Kagere kwenye dakika ya 72 aliyepokea pasi kutoka kwa John Bocco
Licha ya kipigo hicho Yanga inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 58 tofauti ya alama 19 dhidi ya Simba iliyofikisha alama 39
ADVERTISE HERE