Leo Yanga imepoteza mchezo wake wa pili msimu huu ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa watani zao Simba
Ni matokeo ambao yamewaumiza Wana Jangwani lakini ndio mpira wa miguu ulivyo
Licha ya kufungwa, leo Yanga imecheza vizuri zaidi ukilinganisha mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye duru ya kwanza
Juhudi za wachezaji kusaka ushindi hasa kwenye kipindi cha pili zilionekana, ni bahati mbaya matokeo hayakwenda upande wao
Mbio za ubingwa hazijaisha, bado kuna michezo mingi na Yanga bado ina nafasi
Yanga bado ina michezo 14 kumaliza msimu huku wapinzani wao Simba wakiwa na michezo 22
Bado inaongoza ligi kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Azam Fc na alama 19 dhidi ya Simba
Hesabu zitabadilika kama Simba itashinda michezo yote ya viporo, lakini kipigo hiki cha leo hakiiondoi Yanga kwenye mbio za ubingwa
Mchezo unaofuata wa Yanga ni dhidi ya Mbao Fc na utapigwa dimba la CCM Kirumba February 20 kisha kuelekea mkoani Lindi kuikabili Namungo Fc kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 16 bora
Mchezo huo utapigwa February 24 2019