Kocha Mkuu wa Yanga amesema uwepo wake katika klabu ya Yanga hausukumwi na mahitaji ya pesa kwa kuwa amejitosheleza na anafahamu hali ya klabu hiyo kwa sasa
Aidha Zahera amesema hata pesa anazotumia katika klabu hiyo anazitoa kwa mapenzi yake na hahitaji kurudishiwa
"Mimi naweza kufanya kazi hata miaka 10 Yanga bila kulipwa, mimi nilishacheza mpira Ulaya miaka 40 sisubiri ulinipe mshahara tayari nina maisha yangu na biashara zangu nyingi," Zahera ameuambia mtandao wa ShaffihDauda
"Kwangu mpira ni burudani, upo moyoni, sio kwa sababu nina mambo yangu mengine ndio maana nasema hivi hapana.
"Kwa mfano Mourinho analipwa pesa nyingi sana lakini bado anaendelea kutafuta pesa, Messi analipwa pesa nyingi anaweza kucheza bila hata kulipwa lakini kila mwaka anataka kuongezwa pesa."
"Mimi kwangu pesa sio kila kitu, Mungu ametupa zinatusaidia lakini mambo mengine tunapaswa kufanya bila kuweka pesa mbele.
"Mungu alinisaidia kidogo na mimi naisaidia Yanga, siku wakipata pesa hata ikiwa ni miaka 10 baadaye watasema tunadeni kwa mtu fulani wanaweza kuja kunipa"