Azam Fc imeshindwa kuondoka na ushindi mkoani Tanga baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Coastal Union katika moja ya michezo minne ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa leo
Huo ni mchezo wa nne mfululizo Azam Fc inashindwa kushinda nje ya jiji la Dar es salaam
Aidha Mwadui Fc imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United wakati Ruvu Shooting imetoshana nguvu na Kagera Sugar kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Simba imeifunga African Lyon mabao 3-0
Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 58 ikifuatia Azam Fc ambayo imefikisha alama 50
Simba imeendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa na alama 42
Yanga itashuka dimbani kesho Jumatano kuikabili Mbao Fc katika mchezo utakaopigwa dimba la CCM Kirumba