Vilabu vya jijini Dar es salaam vinavyoshiriki ligi kuu vitalazimika kutafuta viwanja vya nyumbani baada ya Serikali kuwa mbioni kufunga uwanja wa Taifa na Ule wa Uhuru kwa ajili ya matengenezo ikiwa ni maandalizi ya fainali za michuano ya AFCON 2019 U17 zitakazofanyika nchini mwezi April 2019
Yanga, Simba, KMC, African Lyon na Ruvu Shooting zimekuwa zikitumia viwanja hivyo na kwa maana hiyo timu hizo zitalazimika kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani
Fainali za michuano hiyo ya vijana zitaanza April 14 na zitamalizika April 18 2019 Tanzania ikishiriki kama mwenyeji wa mashindano hayo
ADVERTISE HERE