Kiungo mkabaji aliyesajiliwa na Yanga kutoka klabu ya Mbabane Swallows Papi Kabamba Tshishimbi amekiri ligi ya Tanzania ina ushindani mkubwa ukilinganisha na huko alikotoka.
Tshishimbi ameichezea Yanga kwenye michezo miwili kwa dakika zote tisini, na muda huo umemtosha kubaini ushindani uliopo kwenye ligi ya Tanzania.
"Ligi ya Tanzania ni ngumu na yenye ushindani mkubwa, hupaswi kudharu timu,unatakiwa kujiandaa vyema kwa kila dakika 90 unazokwenda kuzikabili," Tshishimbi amefunguka.
Akizungumzia mchezo wa Yanga unaofuata dhidi ya Njombe Mji, Tshishimbi amesema Yanga inahitaji kupata ushindi baada ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza.
"Sifikirii kuhusu sare kwenye mchezo uliopita,mimi na wachezaji wenzangu tumejindaa vizuri kwa ajili ya mchezo ujao,tunahitaji kucheza kama mabingwa ili kutetea ubingwa"
Tshishimbi tayari amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye michezo mwili aliyocheza.

ADVERTISE HERE