Kocha wa Yanga, George Lwandamina amerejea jana kutoka kwenye msiba wa baba yake.
Habari mpya ni kwamba ameiambia klabu hiyo iongeze mtaalamu mwingine kwenye benchi la ufundi kulingana na Mwanaspoti
Alichogundua Lwandamina katika kikosi chake ni kwamba washambuliaji wake watatu; Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya, walikuwa na majeruhi kwa muda mrefu wakiuguza tatizo la aina moja, maumivu ya magoti.
Habari za uhakika ambazo Lwandamina mwenyewe kathibitisha ni kwamba kocha huyo ameomba kutafutiwa mtaalamu wa matibabu ya viungo atakayesaidiana na daktari wa timu hiyo Dk. Edward Bavu.
Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema tayari maombi hayo ambayo hata wao wameyakubali, yameshaanza kufanyiwa kazi kwa kumtafuta mtaalamu huyo kwa kuangalia ndani na nje ya nchi atakayefanya kazi hiyo.
Lwandamina alisema: Γ’β¬ΕNikweli nimewaomba wanitafutie huyo mtu, sawa sasa tuna daktari wa timu lakini tunatakiwa sasa kufikiria mbali zaidi kumaliza hali kama hii ya kuwa na wachezaji wengi muhimu majeruhi kama hivi na hili linaweza kuwa tatizo zaidi unapokuwa katika mashindano makubwa ya Afrika ambayo hayana muda wa kupoteza kila mchezo ni muhimu.Γ’β¬Β
Wakati huo huo upo uwezekano winga wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa, Said Maulid 'SMG' akaongezwa kwenye benchi la ufundi la Yanga kwa ajili ya kazi maalumu.
SMG ni mtaalamu wa kukusanya takwimu mbalimbali za wachezaji.

ADVERTISE HERE