Yanga yapendekeza kutumia uwanja wa Samora au CCM Kirumba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2019
Yanga yapendekeza kutumia uwanja wa Samora au CCM Kirumba

Uongozi wa klabu ya Yanga umependekeza kutumia uwanja wa Samora ulioko mkoani Iringa au uwanja wa CCM Kirumba kwa baadhi ya michezo ya ligi itakayochezwa wakati uwanja wa Taifa utakapokuwa umefungwa

Viwanja vya Taifa, Azam Complex na Uhuru vinatarajiwa kufungwa March 24 2019 kupisha ukarabati tayari kwa matumizi katika michuano ya fainali za AFCON 2019 ngazi ya vijana umri chini ya miaka 17

Fainali hizo zitafanyika jijini Dar es salaam kuanzia April 14 mpaka April 28 Tanzania ikiwa mwenyeji

Hata hivyo Bodi ya Ligi Kuu tayari imetangaza kuwa katika kipindi hicho ligi itasimama isipokuwa kwa klabu ya Simba ambayo itaendelea kucheza michezo yake ya viporo iliyopangwa kupigwa nje ya jiji la Dar es salaam

Yanga na timu nyingine zinazotumia viwanja hivyo zimetaarifiwa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani itakayopigwa kati ya March 24 na April 2019

Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wanatarajia kuiandikia barua TFF kuitaarifu uwanja waliouchagua kuutumia kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani

"Tunafahamu Uwanja wa Taifa utafungwa Machi 24, mwaka huu, baada ya mechi ya Uganda mpaka mwezi wa nne, nadhani Mwanza au Iringa inaweza kuwa eneo zuri kwa sababu uwanja ni mzuri na usafiri ni rahisi," Hafidh amenukuliwa na gazeti la Bingwa

Hivi karibuni kocha Mwinyi Zahera alieleza kuvutiwa na uwanja wa CCM Kirumba kutokana na ubora na ukaribu wake kutoka jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege na sapoti kubwa ya mashabiki inayopata Yanga kila inapocheza jijini Mwanza

Zahera pia aliusifia uwanja wa Samora wa mkoani Iringa kuwa unafaa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
54m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’