Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Malangwe Mchungahela na Kamati ya uchaguzi ya Yanga inayoongozwa na Venance Mwamoto (MB), zinatarajiwa kukutana leo
Kikao hicho kinatarajiwa kujadili na baadae kutangaza kuendelea kwa mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Yanga ambapo tarehe ya uchaguzi itatangazwa
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya uchaguzi ya Yanga amesema wamependekeza uchaguzi huo wa kujaza nafasi zilizowazi ufanyike wiki ijayo March 10, 2019
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 13 lakini haukufanyika baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kuuzuia
Nafasi zitakazowaniwa ni ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji
ADVERTISE HERE