Jana wajumbe wa Kamati za uchaguzi za Yanga na TFF walikutana katika kikao ambacho kimehitimisha sintofahamu kuhusu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga ambapo tarehe ya uchaguzi huo itatangazwa leo
Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa katika kikao hicho ni pamoja na kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi ambapo wagombea watalazimika kuchukua fomu upya zoezi ambalo litaanza kesho Alhamisi
Pia kuhusu utata wa Wanchama wenye sifa ya kupiga kura, wanachama walioandikishwa katika leja ya klabu wataruhusiwa kupiga kura bila ya kujali kama wana kadi za kitabu au za benki
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika March 24 2019
ADVERTISE HERE