Viongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga wanatarajiwa kukutana Makao Makuu ya klabu hiyo kuweka mkakati wa uhamasishaji ili kuongeza kasi ya wadau kuchangia
Kutokana na mwenendo wa uchangiaji kuwa taratibu, kukosekana kwa hamasa inatajwa kuwa moja ya sababu inayokwamisha zoezi hilo
"Msimu unaelekea ukingoni, Yanga inahitaji kuwa na fedha ili iweze kutimiza malengo yake kama alivyoainisha kocha Mwinyi Zahera," amesema Edwin Kaisi kiongozi wa Matawi ya jijini Dar es salaam
"Kama tutashindwa kupata kiasi cha fedha kinachotakiwa basi huenda msimu ujao tukawa na wakati mgumu zaidi. Ni lazima tuhamasishane ili kila anayeweza achangie kwa kiwango anachomudu"
Viongozi hao wamemualika kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samwel Lukumay