Ten afunguka usajili wa Ndemla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2019
Ten afunguka usajili wa Ndemla

Kwa siku za karibuni kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amekuwa akimposti kiungo wa Simba Said Khamis Ndemla huku akiweka jumbe zinazoashiria kuwa huenda mabingwa hao wa kihistoria wanaiwania sahihi ya kiungo huyo kwa ajili ya msimu ujao

Ndemla nusura asajiliwe na Yanga katika usajili wa mwanzoni mwa msimu huu kabla hajaamua kubaki Simba kwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja

Jana Ten alifunguka kuhusu tetesi za Yanga kumuwania Ndemla ambapo amekiri kuwa kiungo huyo ana uwezo mkubwa lakini ana bahati mbaya hapati nafasi katika klabu yake ya Simba

"Ndemla ni mchezaji mzuri sana. Mtu yeyote ukimuuliza katika wachezaji wa Tanzania wenye vipaji hawezi kukosa kumtaja Ndemla," amesema Ten

"Ndemla mimi ni rafiki yangu, suala la kusajili au kutosajiliwa na Yanga hilo linahusu benchi la ufundi na Kamati yetu ya usajili. "

"Yote yanaweza kusemwa mwisho wa msimu lakini kwa sasa hivi huwezi kuzungumza lolote lakini anabaki kuwa ni mchezaji mwenye kipaji na kila mtu anaona"

"Amekuwa ni mchezaji mwenye mwenendo mzuri licha ya kuwa sasa hapati nafasi kwenye timu yake"

Wakati msimu ukielekea ukingoni tayari timu zimeanza 'kupigana vikumbo' kuwania wachezajia ambao mikataba yao inaelekea ukingoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’