Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kuondoka nchini keshokutwa Jumanne kuelekea kwao DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa
Zahera ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo, amesema timu hiyo inakabiliwa na mchezo mgumu wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 dhidi ya Libya
Zahera aliyeiongoza Yanga leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, amesema kocha msaidizi Noel Mwandila atawajibika kukiongoza kikosi cha Yanga wakati wote ambao hatakuwepo
Mchezo unaofuata wa Yanga ni ugenini mkoani Iringa dhidi ya Lipuli Fc, Jumamosi ijayo March 16 2019
ADVERTISE HERE