Haruna Niyonzima ameitumikia Yanga kwa misimu sita na katika kipindi hicho Yanga imepata mafanikio makubwa kwa kutwaa mataji manne ya VPL.
Hakuna mwenye shaka juu ya uwezo wake, lakini ni lazima kukubaliana inapofika wakati mtu anataka kwenda kujaribu mahali pengine.
Ukweli ni kwamba Niyonzima alikuwa akiipenda sana Yanga na ni kweli hakuwa amesaini Simba wakati ikidaiwa tayari amefanya hivyo.
Niyonzima aliahidi akirudi kutoka Rwanda alikokuwa amekwenda kuitumikia timu ya Taifa, angesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga kulingana na makubaliano ambayo yalikuwa yamefikiwa.
Juzi tulitoa taarifa hapa kwamba tayari amesaini miaka miwili, hiyo ilikuwa taarifa tuliyokuwa tumeipata kutoka kwa mmoja wa viongozi.
Lakini inaelezwa kuwa Niyonzima aligeuka dakika za mwisho wakati anatakiwa asaini mkataba akitaka aongezwe pesa ya usajili.
Na hii ni kutokana na ukweli kwamba Simba walikuwa wamemuwekea mezani ofa ya Mil 100.
Sasa akataka apewe zaidi ya Mil 100 au la aachwe aende anakokutaka.
Niyonzima alikuwa na thamani hiyo ya zaidi ya Mil 100 wakati tunamsajili miaka sita iliyopita lakini si sasa.
Ni kweli timu yetu inataka kuwabakisha wachezaji wetu muhimu lakini ni uamuzi sahihi kwa uongozi kutoa pesa kulingana na thamani ya mchezaji husika kwa wakati sio kutoa pesa tu eti kwa kuwa mchezaji ametishia kujiunga na timu pinzani.
Kwa wale msioifahamu vizuri Yanga haina mambo ya kubembelezana. Klabu hii ilishawahi kutimua wachezaji wa kikosi kizima na kuanza upya na bado ikapata mafanikio.
Na mfahamu sio Niyonzima tu, kuna wachezaji wengine muhimu huenda wataachwa kwa kuwa wanataka pesa nyingi ili wasaini mikataba mipya.
Tumtakie kila la kheri Niyonzima huko aendako maisha ni lazima yaendelee.

ADVERTISE HERE