Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wametozwa faini ya jumla ya sh. 6,000,000 (milioni sita) kutokana na makosa waliyofanya kwenye mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Februari 16 2019
Yanga imeadhibiwa kwa tukio la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji wakaguliwe kwenye korido.
Pia kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch) katika mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Nayo Simba imetozwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) baada ya kuingia uwanjani kwenye mchezo huo wakitumia mlango usio rasmi, lakini vilevile kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch).