Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja huo kesho Jumamosi, March 16 2019
Meneja wa Yanga Nadir Haroub amesema wachezaji wa timu hiyo waliosafiri mkoani iringa wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa Iringa na maeneo ya jirani






ADVERTISE HERE