Kamusoko afunguka kipigo cha Lipuli Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Mar 2019
Kamusoko afunguka kipigo cha Lipuli Fc

Aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Yanga kwenye mchezo dhidi ya Lipuli Fc Thabani Kamusoko amesema wamekubaliana na matokeo ya kufungwa bao 1-0 jana na wanajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuatia

Kamusoko amesema licha ya jitihada walizofanya, walishindwa kuutumbukiza mpira kimiani kupitia nafasi nyingi walizotengeneza

"Bahati haikuwa upande wetu. Wenzetu wamepata nafasi moja wameitumia sisi tumeshindwa kutumia nafasi nyingi tulizotengeneza," amesema

"Benchi la ufundi limeona mapungufu yaliyojitokeza, naamini yatafanyiwa kazi mazoezini ili kuhakikisha tunapata matokeo kwenye mchezo utakaofuatia"

Katika mchezo huo Kamusoko alitolewa kwenye kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Amissi Tambwe

Winga Deus Kaseke alipata nafasi adimu ya kubaki yeye na mlinda lango lakini akashindwa kuutumbukiza mpira kimiani

Baada ya kupata bao la mapema kwenye dakika ya 20, Lipuli Fc ilicheza kwa kujihami zaidi na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa Yanga kuweza kuipenya ngome yao ya ulinzi iliyokuwa na wachezaji wengi

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo

Kituo kinachofuatia ni mkoani Mtwara ambapo April 03 Yanga itakuwa ugenini dhidi ya Ndanda Fc

Hata hivyo kabla ya mchezo huo, Yanga itacheza na Alliance Fc katika mchezo wa robo fainali kombe la FA utakaopigwa kati ya March 25-28 2019

Baada ya kukamilika kwa michezo ya mzunguuko wa 31, ligi itasimama kupisha michezo ya mwisho ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za AFCON 2019

Michezo hiyo itapigwa kati ya March 23-25 2019

Taifa Stars itashuka dimba la Taifa April 24 kuikabili Uganda Cranes katika mchezo ambao matokeo ya ushindi ni lazima kwa Stars huku pia ikiomba Lesotho isipate ushindi ugenini dhidi ya Cape Verde

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’