Uongozi wa Yanga unakusudia kuanzisha utaratibu wa kukaribisha msimu mpya kwa kuwakutanisha Wana Yanga katika tukio ambalo pia litatumika kutambulisha wachezaji wapya, jezi na bidhaa nyingine za klabu
Baada ya klabu ya Simba kuwa na utaratibu huo kwa misimu kadhaa, wadau wamekuwa wakitoa ushauri kuwa si vibaya kwa Yanga nayo kuanzisha mfumo huo kwani ukiachilia mbali kutumika kuwakutanisha wadau, timu itanufaika kutokana na mapato yatakayopatikana
Tayari uongozi wa Yanga umeanza maandalizi ya mikakati hiyo yenye lengo la kuisogeza Yanga karibu zaidi na wadau wake
ADVERTISE HERE