Kamati Maalum yaongeza watia saini fedha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2019
Kamati Maalum yaongeza watia saini fedha Yanga

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Yanga Mh Anthony Mavunde amesema nahodha Ibrahim Ajib na Kocha Mwinyi Zahera hawajaondolewa kutia saini katika Akaunti Maalum iliyofunguliwa kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha kikosi cha timu hiyo

Mavunde ameiambia Yanga TV kuwa Ajib na Zahera watabaki kuwa watia saini kutokana na umuhimu wao

"Lazima kapteni na kocha waendelee kubaki kuwa watia saini sababu hawa ni watu muhimu sana," amesema Mavunde

Aidha ili kuongeza uaminifu na kuwahakikishia Wanayanga kuwa fedha wanazochangia ziko salama, Mavunde amesema Kamati imependekeza kuongeza watia saini wengine ambao ni Mhasibu wa klabu na kiongozi mmoja wa Yanga

Pia Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ambao ndio wanaongoza zoezi la kutafuta fedha nao watakuwa miongoni mwa watia saini

"Lakini pia viongozi waliopo, kwa maana mtaalamu wetu ambaye ni mhasibu na kiongozi mmoja wa Yanga nao watakuwepo sehemu ya watia saini"

"La tatu ni kundi la Kamati yenyewe ambao kimsingi ndio watafuta fedha, Mwenyekiti nitakuwepo miongoni mwa watia saini na Makamu Mwenyekiti"

"Hii yote tunaifanya katika kuongeza uwajibikaji na vilevile tuishi kwenye misingi ya uadilifu mkubwa ili fedha inayochangwa na Mwanayanga iende kufanya kazi iliyokusudiwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’