Mchakato wa uchaguzi wa Yanga unasubiri kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu hiyo
Kufuatia mapendekezo ya Baraza la Wadhamini, Yanga itafanya uchaguzi wa kujaza nafasi zote uchaguzi ambao ulipaswa kufanyika mwakani
Wajumbe wa Baraza la Wadhamini Yanga, Kamati ya uchaguzi ya TFF na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wanatarajiwa kukutana katika kikao ambacho kitatoa muongozo wa mchakato huo hasa sintofahamu kuhusu wagombea ambao tayari waliteuliwa kugombea nafasi zilizokuwa wazi katika uchaguzi uliopaswa kufanyika Januari 13 2019
Kwa kuwa Yanga imeamua kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zote, huenda mchakato huo ukaanza upya kwa wagombea kutakiwa kujaza fomu
Yanga imeshauriwa kuharakisha kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi ili kupata viongozi wapya ambao wataweza kusimamia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo