KMC na Lipuli Fc zimekuwa timu za kwanza kutinga nusu fainali kombe la FA (ASFC) baada ya kushinda michezo yao ya robo fainali iliyopigwa leo
Lipuli Fc imeichapa Singida United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Samora wakati KMC nayo imeilaza African Lyon mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo
Hatua ya nusu fainali KMC itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam Fc utakaopigwa keshokutwa Ijumaa
Wakati Lipuli Fc itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Alliance Fc dhidi ya Yanga, mchezo wa nusu fainali utapigwa uwanja wa Samora
ADVERTISE HERE