Kindoki afichua siri ya ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2019
Kindoki afichua siri ya ubora wake

Mlinda lango wa Yanga Klausi Kindoki, ametoa siri ya kuimarika kwa kiwango chake kuwa ni kuacha kusikiliza kelele za wanaombeza na kufanya mazoezi kwa bidii.

Kipa huyo juzi aliibuka shujaa kwa kupangua penalti mbili, ikiwamo ya mwisho katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) dhidi ya Alliance na kuiwezesha Yanga kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, timu hizo ziliingia katika mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90, hivyo Yanga kuibuka na ushindi wa penalti 4-3.

Kindoki alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea DR Congo, lakini kwa muda mrefu amekuwa hakubaliki kwa mashabiki wa kikosi hicho.

Kindoki ambaye amepita katika kipindi kigumu, amesema kwa sasa anachoangalia ni kazi yake bila kujali watu wanasema nini.

Amesema siku zote alikuwa anajiamini kuwa ni kipa mzuri na ipo siku atakubalika na kufanya kile mashabiki wa timu yake wachohitaji bila kukata tamaa.

"Sasa hivi nimeacha kufuatilia wale wanaonisema vibaya, ninafanya mazoezi kwa bidii sana na kuondoa presha ninapoingia uwanjani, unajua Yanga ina mashabiki wengi kuliko timu niliyokuwa nachezea kule Congo (DRC), Kindoki amenukuliwa na gazeti la Bingwa"

"Nina furaha kwa sasa, ninachowaambia mashabiki wa Yanga wawe na imani na mimi, kwani huo ni mwanzo na watafurahi zaidi ya hapo.

"Nitafanya mazoezi na kujituma zaidi uwanjani, nataka kuiona Yanga ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Federationa Cup) na kuchukua ubingwa," amesema Kindoki.

Akizungumzia jinsi alivyofanikiwa kuivusha timu yake hatua ya nusu fainali ya ASFC, alisema kabla hawajaingia katika kupiga penalti, kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, alimwambia aangalie mpira vizuri na kuondoa hofu.

"Nilizungumza na kocha kabla ya penalti na nimefanya kile alichoniambia, nimefuhi sana kufanikiwa kutoa zile penalti kwa sababu mchezo ulikuwa ni mgumu"

Alieleza kuwa kingine kilichomfurahisha ni kitendo cha mashabiki wa soka kumwimbia wakitaja jina lake, kwani ni mara ya kwanza inatokea tangu ametua katika kikosi hicho.

Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’