Tujilaumu wenyewe kwa kukosa ushindi dhidi ya Ndanda Fc - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2019
Tujilaumu wenyewe kwa kukosa ushindi dhidi ya Ndanda Fc - Zahera

Kocha Yanga, Mwinyi Zahera amesema matokeo ya sare 1-1, dhidi ya Ndanda waliyoyapata katika mechi ya leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara wameyataka wenyewe.

Zahera alisema hata kiwango ambacho alikionesha refa wa mchezo huo Martin Sanya kilikuwa kizuri na hata wale watu ambao wanamlaumu kuwa alifanya makosa katika mchezo huo kwake wala hayakuyaona.

Alisema wachezaji wangu walifanya makosa kipindi cha kwanza ambayo ilikuwa lazima Ndanda waweze kuyatumia na waliweza kufanya hivyo kwa kutumia moja kati ya waliozipata.

"Uwanja pia si mzuri haswa katika eneo la kuchezea nao naweza kusema ulichangia timu yangu kushindwa kucheza vizuri na kushindwa kupata pointi tatu ambazo ndio yalikuwa malengo yetu na tukashindwa kufanya hivyo tukapata matokeo haya," alisema.

"Katika kipindi cha kwanza hatukuwa tunacheza kwa kuchangamka na kushambulia kwa haraka kwani tulikuwa tunacheza na timu ya chini kwenye msimamo jambo ambalo walituzoea na kuja kwetu kutushambulia kwa haraka.

"Timu kama Ndanda ilibidi tuwape presha kama tulivyofanya katika kipindi cha pili ili wafanye makosa ambayo yangetupa mianya ya kufunga bao zaidi ya moja ambalo tulilipata kipindi cha pili," alisema Zahera.

Yanga walisawazisha bao kipindi cha pili dakika 61, kupitia kiungo Tshishimbi kwa kichwa akipokea krosi ya beki wa kati Kelvin Yondani.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’