Wakati Kamati Maalum ya uhamasishaji ikitarajiwa kuzindua rasmi kampeni ya uchangiaji wa Yanga, wapenzi, mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo wamesisitiziwa kuendelea kuichangia timu ili kuhakikisha malengo yaliyopangwa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Anthony Mavunde amesema fedha zitakazochangishwa sasa zitasaidia kukiboresha kikosi cha Yanga pamoja na kupatikana fedha za kulipa mishahara kwa angalau miezi sita
"Huu ni Mpango wa Muda wa kati, Zoezi letu sasa ni kumkusanyia fedha Mwalimu ili asajili kikosi shindani na pia tuwe na uwezo wa kulipa mishahara takribani kwa miezi 6 wakati Uongozi Mpya ukijipanga," amesema
Kamati ya Mavunde imeweka mkakati wa kukusanya angalau Tsh Bil 1.5 hadi kufikia mwisho wa mwezi huu
ADVERTISE HERE