Mwandila alia na uchovu wa wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya African Lyon

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2019
Mwandila alia na uchovu wa wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya African Lyon

Kikosi cha Yanga kiko jijini Mwanza kikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa CCM Kirumba

Kabla ya kutua Mwanza, Yanga ilitokea mkoani Mtwara ambako ilicheza na Ndanda Fc na kulazimishwa sare ya bao 1-1

Vinara hao wa ligi kuu wamepata siku mbili tu za kujiandaa kabla ya kuivaa African Lyon hapo kesho

Kocha Msaidizi Noel Mwandila amesema licha ya kutopata muda wa kutosha wa kufanya maandalizi kutokana na ratiba, amesema wamepania kushinda mchezo dhidi ya African Lyon

"Hatujapata muda wa kutosha kujiandaa, maana baada ya mchezo dhidi ya Ndanda Siku ya ijumaa tukarejea Dar kisha siku inayofuata tukawasili Mwanza"

"Kwa hiyo siku mbili zote zimekuwa ni kwa ajili ya safari tu, hata leo hatuwezi kufanya mazoezi zaidi ni kuandaa miili na kuondoa uchovu," amesema

"Mchezo uliopita tulidondosha alama mbili lakini kesho ni matumaini yangu tutaibuka na ushindi ukizingatia vijana wana morali na ari ya ushindi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’