FT : Yanga 2-0 African Lyon

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Apr 2019
FT : Yanga 2-0 African Lyon

Vinara wa ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga wameendelea kujichimbia kilelenimwa msimamo wa ligi baada ya kuifumua African Lyon mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda Fc katika mchezo uliopita, vijana wa Yanga leo waliingia CCM Kirumba wakiwa na shauku ya kuondoka na alama zote tatu

Iliwachukua dakika tano tu kuandika bao la kuongoza kupitia kwa kinara wake wa mabao Heritier Makambo aliyeunganisha nyavuni pasi 'mvusho' iliyopigwa na Kelvin Yondani

Makambo akaiongezea Yanga bao la pili kwenye dakika ya 31 akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa Haruna Moshi.

Makambo amefikisha mabao 14 na kuchupa hadi nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa upachikaji mabao akiwa sawa na Meddie Kagere wa Simba

Yanga ingeweza kufunga mabao zaidi kama wachezaji wake wangekuwa makini katika lango la African Lyon

Hata hivyo ushindi huo umeihakikishia Yanga kibaki kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Azam Fc baada ya kufikisha alama 71

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’