Kibadeni apongeza zoezi la uchangiaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
8 Apr 2019
Kibadeni apongeza zoezi la uchangiaji Yanga

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni, ameipa tano klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha kujitokeza hadharani kuomba msaada wa kifedha kwa wanachama na mashabiki wao, akikiita ni cha kishujaa.

Kibadeni amesema viongozi wa Yanga wamefanya jambo kubwa na la kihistoria na linaweza kuwapa matunda mazuri na kuwa somo kwa klabu nyinginezo.

“Tumeona baadhi ya timu za Ligi Kuu na hata Ligi Daraja la Kwanza zikidai hazina uwezo wa kifedha, lakini hawajafanya tukio kama la Yanga," Kibadeni ameliambia gazeti la Bingwa

“Unapoamua kuandaa tukio maalumu kwa ajili ya kuchangia kitu hata yule ambaye hakuwa tayari kuwachangia, anashawishika kuwasaidia, binafsi nawapongeza sana Yanga kwa hili,” alisema.

“Watanzania tumekuwa na kawaida ya kudharau kidogo na kukipa uzito kikubwa cha mara moja huku tukisahau kuwa kile tunachokiona si kitu, kina uwezo wa kuwa na uzito sawa na tunachokithamini.

“Timu nyingine zinapaswa kuwaiga Yanga, ninauhakika wanachama na mashabiki wana nguvu kubwa ya kuisaidia timu yao kuliko makampuni au taasisi ambazo nyingine zina masharti magumu,” alisema.

Yanga kupitia kamati yake Maalum ya kuratibu zoezi la uchangiaji, ilijiwekea malengo ya kukusanya Tsh Bilioni 1.5 ambapo Kamati hiyo imesema tayari imefanikiwa kwa asilimia 90

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →