Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani leo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake waliokuwa wakijifua kwenye uwanja wa CCM Kirumba kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Alhamisi, April 11 2019
Yondani alipata majeraha jana katika mchezo dhidi ya African Lyon, mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Hata hivyo beki Abdallah Shaibu 'Ninja' amemaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu hivyo anaweza kuchukua nafasi ya Yondani kama mkongwe huyo atashindwa kurejea dimbani mapema
ADVERTISE HERE