Kamat ya uchaguzi ya Yanga na ile ya TFF leo zimekutana Makao Makuu ya Yanga na kufanya mchujo wa awali wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo
Kikao hicho kimewapitisha wagombea wote, hata hivyo kimewataka wakamilishe baadhi ya nyaraka ambazo zimekosekana katika fomu zao
Wametakiwa kufika na nyaraka hizo siku ya usaili ambao utafanyika April 14-16, 2019
Nyaraka hizo ni Cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha Taifa, Vyeti halisi vya elimu na kadi ya uanachama wa klabu ya Yanga
Wagombea watakaofuzu usaili huo watajumuishwa na wale ambao walipitishwa katika mchakato wa uchaguzi wa nafasi zilizowazi

ADVERTISE HERE