Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga Dismas Ten amesema klabu hiyo ina thamani ya Tsh Bilioni 120
Mwishoni mwa mwaka 2017 Yanga iliunda Kamati ya Mabadiliko iliyoongozwa na Mwenyekiti Alex Mgongolwa ambapo jukumu la kwanza la Kamati hiyo ilikuwa kufanya tathmini ya mali za Yanga na kubaini thamani ya klabu hiyo
"Kwa mujibu wa taarifa na hesabu zilizopo mezani, thamani ya Yanga ni Tsh bilioni 120, ikiwa na gawanyo la bilioni 30 kwa Kila miezi 3 katika miezi 12 inayounda mwaka mzima," ameandika Ten kwenye mtandao wa Instagram
"Kwenye hili najua wengi hawataelewa ila wachache wataelewa, acha tusubiri uchaguzi upite"
Inaelezwa baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi na Yanga kupata viongozi wapya mwezi ujao, mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji utaanza