Bado hatujakata tamaa ya ubingwa ligi kuu - Dante

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2019
Bado hatujakata tamaa ya ubingwa ligi kuu - Dante

Mlinzi wa kati wa Yanga Andrew Vicent 'Dante' amesema watahakikisha wanashinda michezo yote nane iliyobaki ili kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa

Yanga inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 71 baada ya kushuka dimbani mara 30 ikifuatiwa na Azam Fc yenye alama 63 ikiwa imeshuka dimbani mara 30 pia

Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 57 baada ya kushuka dimbani mara 22

Kama Yanga itashinda michezo yote nane iliyobaki, itafikisha alama 95

"Hatutakiwi kuvipigia hesabu viporo vya Simba, tunapaswa kushinda mechi zilizobakia ili kuishi malengo yetu, Yanga tuna nafasi kubwa ya ubingwa kwani hakuna anayejua matokeo kabla ya mechi," Dante amenukuliwa na Mwanaspoti

"Tumeshinda dhidi ya African Lyon ni kitu kizuri kwetu kwani kinakuwa kinaendelea kutuweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi kuu Bara.

"Lakini pia tunaelekeza nguvu kwenye michuano ya FA, kuhakikisha tunapata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa mwakani"

Licha ya Simba kuwa na michezo mingi ya viporo, inabanwa na muda mchache uliobaki kuelekea ligi kumalizika kwani itahitaji kucheza michezo yake mfululizo ili kuwezesha ligi hiyo kumalizika kwa wakati

Wakati baadhi ya timu zikisalia na michezo mitano hadi nane, Simba itahitaji kushuka dimbani mara 16 katika kipindi cha mwezi mmoja na siku kadhaa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’