Matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom hayakufurahiwa na kila mmoja wakiwemo wachezaji na benchi zima la ufundi.
Kocha George Lwandamina alipata msiba mzubwa wa kufiwa na baba yake lakini alirejea jijini Dar es salaam siku tatu baadae kuhakikisha anakiandaa vyema kikosi chake kipate ushindi katika mchezo ujao dhidi ya Njombe keshokutwa Septemba 10.
Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa moja ya kauli yake kuelekea mchezo huo alisema klabu imeyafanyia kazi matatizo ya ufungaji yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza na sasa Yanga iko tayari kupata ushindi katika mchezo huo.
Katika mchezo huo pia huenda Yanga ikapata huduma ya mshambuliaji wake msumbufu Obrey Chirwa aliyekuwa nje kwa zaidi ya wiki sita kutokana na majeruhi.
Mchezo huo ni wa kufa au kupona kwa Yanga. Matokeo tofauti na ushindi yanaweza kuamsha hisia za mshabiki wa Yanga dhidi ya kocha George Lwandamina.
Lwandamina analifahamu hilo, nadhani keshokutwa Jumapili moto utawaka kwenye dimba la sabasaba mkoani Njombe.

ADVERTISE HERE