Mkongwe Yanga awapa somo wanachama kuelekea uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2019
Mkongwe Yanga awapa somo wanachama kuelekea uchaguzi

Maamuzi ya Yanga kufanya uchaguzi mkuu Mei 5, yanatajwa ni mapinduzi mapya ya kiuchumi, kimtazamo na mawazo ndani ya klabu hiyo, tofauti na hali ambayo wanapitia kwa sasa.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Bakari Malima β€˜Jembe Ulaya’ alisema uchaguzi huo ulenge kuwapata watu sahihi ambao, watakuwa na nia ya kuipeleka Yanga kwenye ushindani wa kimataifa.

"Simba imara inahitaji Yanga imara kwa sababu klabu hizi mbili ni kioo cha soka la Tanzania huo ndio ukweli, uchaguzi utakaofanyika Mei 5 kwa Yanga uwe wa mapinduzi ya kuleta vitu tofauti na vyenye tija sio kama miaka iliopita.

"Natamani ziingie sura mpya na sio wale ambao walikuwepo kwenye uongozi wa nyuma kwani, hawakuweza kufanya kitu chochote.

"Yanga tunahitaji ifike mbali na sio ilivyo kwa sasa mpaka inafikia mahali tunachangishana, klabu hiyo ni tajiri hapa vije vichwa vya kufanya mambo.

"Wanaochagua viongozi waache tamaa za kuchukua posho za wagombea, hilo limewahi kunikuta uchaguzi uliopita niligombea ujumbe watu wanataka niwape pesa natoa wapi sasa. nilipata kura 577, hivyo sikupita kwani walitakiwa 10 tu mimi nilikuwa wa 11.

"Uchumi ndio kikwazo cha wachezaji wa zamani tushindwe kwenda kuchukua fomu ili kusaidia klabu kuwa na soka la mfano, lakini yote kwa yote waje watu makini ambao, wana uwezo wa kubuni mikakati mipya ili kuhakikisha Yanga inafika mbali tofauti na mambo yalivyo sasa"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
16h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
20h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
21h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
21h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’