Chambua ataka sura mpya uongozi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2019
Chambua ataka sura mpya uongozi Yanga

Nyota wa zamani wa Yanga 'legendary' Sekilojo Chambua amesema wanachama wa klabu hiyo wanahitaji kuchagua viongozi wapya ambao wataipa mafanikio klabu hiyo

Aidha Chambua ameshangazwa na baadhi ya wagombea ambao walikuwa viongozi kurudi tena kwenye kinyang'anyiro licha ya kushindwa kutumia vyema nafasi walizokuwa nazo awali

Chambua ambaye ni Mwanachama wa Yanga, amewataka wanachama wenzake kuwa makini katika kampeni kwa kusikiliza hoja za wagombea ambazo zinatakiwa kulenga mabadiliko ambayo yanaweza kuivusha klabu kutoka katika mfumo wa kuwa tegemezi na kuingia katika mfumo wa uendeshwaji wa kujitegemea.

"Yanga ni klabu kubwa inahitaji kupata viongozi wenye upeo mkubwa wa kuifanya iwe mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi, watakaoweza kufanya hivyo ni watu wapya ambao watakuja na mawazo mapya na siyo viongozi waliopita miaka ya nyuma na kushindwa kuifanya timu ikawa na mifumo bora," Chambua amenukuliwa na Mwanaspoti

"Tulikuwa na mfumo wa kumtegemea tajiri mmoja, ameondoka unaona kabisa timu ilivyoyumba na kukosa ubora wa kiushindani. "

"Sidhani kama kuna wanachama wanapendezewa na hili, hivyo naomba iwe changamoto kwetu kuhakikisha tunachagua kiongozi bora na mwenye nia nzuri ya kuivusha klabu kutoka hapa ilipo na kuipeleka sehemu nyingine”

"Inashangaza kuona viongozi wameitumikia timu kwa muda mrefu bila mafanikio wanarudi tena na ndiyo maana nawasisitiza kuwa makini katika hili kwa kusikiliza zaidi hoja za watu wapya, kwani waliokuwepo mwanzoni walishindwa wapi kama wanataka kurudi tena kwa mara nyingine?" alihoji.

Mchakato wa uchaguzi wa Yanga uko katika hatua ya mchujo wa wagombea ambapo leo Kamati ya uchaguzi huenda ikaweka hadharani majina ya wagombea wenye sifa ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo

Uchaguzi utafanyika May 05 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’