Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amelalamikia mabadiliko ya muda wa mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka saa 10:00 jioni na kurudishwa nyuma hadi saa 8:00 mchana
"Mambo ya AFCON hayajaja jana, ilikuwa inajulikana muda mrefu na ratiba ya mechi yetu na Mtibwa ilikuwa inajulikana tangu zamani lakini wanasubiri hadi siku moja kabla ya mechi wanasema mechi itachezwa saa 8 mchana," Zahera aliuambia mtandao wa ShaffihDauda
"Walipaswa kuangalia wakati wanapanga ratiba za AFCON wangepanga na mechi za ligi ili wapishanishe siku zinazochezwa mechi za ligi kusiwe na mechi za AFCON. Watu wanaamka tu na kuamua."
"Kucheza saa nane mchana inabidi wachezaji wawe wameandaliwa kucheza muda huo na wawe wamezoea kwa kipindi fulani kwa sababu inabidi hadi ratiba ya chakula ibadilike kulingana na muda wa mechi."
Mechi zote za ligi kuu zinazochezwa leo zitapigwa saa nane mchana