Chirwa kuongoza mashambulizi ya Yanga kesho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Sep 2017
Chirwa kuongoza mashambulizi ya Yanga kesho
Mshambuliaji Obrey Chirwa anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Yanga kitakachoivaa Njombe Mji katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa Jumapili, Septemba 10 kwenye dimba la Sabasaba Njombe.

Chirwa hajaitumikia Yanga kwa zaidi ya wiki sita kutokana na majeruhi lakini sasa imeelezwa mchezaji huyo yuko tayari kurejea dimbani.

Meneja wa Yanga Hafidhi Saleh amesema kikosi cha Yanga kilifika salama mkoani Njombe, Chirwa akiwa miongoni mwa wachezaji walio kikosini.

Amesema daktari wa timu amewahakikishia kuwa Chirwa yuko fiti hivyo ni uamuzi wa kocha Lwandamina kumpanga au la.

Kwa maana hiyo tutarajie Chirwa, Ngoma na Ajib kuongoza mashambulizi ya kikosi cha Yanga kinachohitaji ushindi katika mchezo huo.

Pius Buswita ni mchezaji mwingine ambaye anaweza kurejea kikosini baada ya adhabu yake ya kufungiwa mwaka mmoja kutenguliwa na TFF.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’