Mzee Akilimali ashusha panga chini, asema atachinja mbuzi baada ya uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2019
Mzee Akilimali ashusha panga chini, asema atachinja mbuzi baada ya uchaguzi

Mzee Ibrahim Akilimali ni Mwanachama maarufu wa Yanga ambaye anafahamika sana kwani amekuwa kinara wa kupaza sauti pale anapoona mambo hayaendi sawa

Wakati mwingine alionekana kwenda kinyume na Wanachama wenzake wa Yanga hivyo kujikuta akiingia kwenye mivutano ya hapa na pale

Lakini hili la uchaguzi limemfurahisha Katibu huyo wa Baraza la Wazee Yanga ambapo amesema atachinja Mbuzi baada ya Yanga kupata viongozi wapya

Mzee Akilimali amesema tatizo kubwa la Yanga ni uongozi lakini sasa baada ya uchaguzi anaamini viongozi watakaopatikana wataweza kumaliza changamoto zinazoikabili timu hiyo

"Tunahitaji viongozi ambao wanajua thamani ya nembo yetu ya Yanga"

"Nachukizwa na mambo ya kupitisha bakuli ni aibu kwetu na hiyo yote inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kutokuwepo viongozi," Mzee Akilimali amenukuliwa na Mwanaspoti

"Uwepo wa viongozi ungeweza kutukwamua kwenye aibu ya kuchangishana"

"Sisemi kuwa ni vibaya wanachama kuichangia klabu, lakini kwa ukubwa wa Yanga si vema kutegemea fedha kutoka kwa wanachama peke yake"

"Nitafurahi na kuwaunga mkono viongozi ambao kwa pamoja wanayanga tutawapa ridhaa ya kutuongoza. Kwa namna mchakato wa uchaguzi unavyoenda nadhani tutapata viongozi bora"

Yanga itafanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya katika kipindi cha wiki mbili zijazo, May 05 2019

Baada ya wagombea waliokuwa viongozi awamu iliyopita kuondolewa kwenye mchakato baada ya kuwekewa mapingamizi, sura mpya zinatarajiwa kuchaguliwa kuiongoza Yanga kwa kipindi cha miaka minne

Inaelezwa moja ya mikakati ya Yanga baada ya kupata viongozi wapya ni kukamilisha mchakato wa mabadiliko kwa kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo ambao kimsingi tayari ulishapitishwa na Wanachama wa klabu hiyo

Kwa sasa Yanga inawashirikisha mashabiki na wanachama wake kuichangia ili iweze kuvuka salama katika kipindi cha mpito

Yanga inahitaji fedha za kuboresha kikosi chake kwa kufanya usajili wa wachezaji wapya pamoja na kuwa na fedha za kulipa mishahara ya wachezaji angalau kwa msimu wote ujao wakati uongozi mpya ukiendelea na mchakato wa mabadiliko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’