Zahera ana haki ya kulalamika, waamuzi wameigharimu Yanga msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2019
Zahera ana haki ya kulalamika, waamuzi wameigharimu Yanga msimu huu

Juzi mwamuzi mstaafu Othman Kazi alimaliza utata wa kukataliwa kwa bao halali la Yanga lililofungwa na Amissi Tambwe kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa uwanja wa Jamhuri

Kupitia kipindi chake cha Kipenga, Kazi aliainisha jinsi waamuzi walivyoinyima Yanga bao halali

Lakini tukio la juzi sio la kwanza kwa Yanga kukumbana na maamuzi ya 'hovyo' yaliyoigahrimu timu hiyo matokeo muhimu

Rejea michezo dhidi ya Coastal Union na Singida United ambayo Yanga ilinyimwa mabao halali ambayo pia Kazi aliwahi kuyafanyia uchambuzi kwenye kipindi hicho. Achilia mbali michezo mingine ambayo Yanga ilishinda licha ya mabao yake mengine kukataliwa

Juzi baada ya mchezo kocha Mwinyi Zahera aliwalalamikia waamuzi kwa kuendelea kuinyima timu yake matokeo huku hali ikiwa tofauti kwa wapinzani wake katika mbio za ubingwa Simba ambao wamekuwa wakinufaika zaidi na matukio ya utata

Zahera alisema matukio haya yamekuwa yakifanywa na waamuzi bila ya wasimamizi wa mpira kuchukua hatua yoyote. Kwa tathmini yake Zahera alisema mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ulikuwa wa tano kwa Yanga kunyimwa matokeo

Kinachoshangaza zaidi ni Yanga kuwa muathirika mkubwa wa matukio hayo ya mabao halali kukataliwa kuliko timu nyingine

Zahera alilamikia utaratibu huu wa kuzikwamisha baadhi ya timu na kuzinufaisha nyingine kuwa hauwezi kulisaidia soka la Tanzania

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’