Mchezo wa nusu fainali kombe la FA (ASFC) kati ya Lipuli Fc dhidi ya Yanga utapigwa May 06 siku moja baada ya uchaguzi Mkuu wa Yanga
Yanga iliyopania kutwaa kombe la FA, itasafiri kwenda mkoani Iringa kuwakabili Wana Paluhengo hao ambao walipata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi uliopigwa katika uwanja wao
Aidha kabla ya mchezo huo Yanga inakabiliwa na michezo miwili ya ligi
April 29 itachuana na Azam Fc mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa kisha kurejea katika uwanja huo May 02 kuikabili Tanzania Prisons
May 10 Yanga itasafiri mkoani Mara kuikabili Biashara United kabla ya kurejea jijini Dar es salaam May 14 kuikabili Ruvu Shooting
ADVERTISE HERE