Lunyamila atia neno uchaguzi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2019
Lunyamila atia neno uchaguzi Yanga

Wanachama wa Yanga wanaojiandaa kuchagua viongozi wapya kwenye Uchaguzi Mkuu wao utakaofanyika Mei 5, wametahadharishwa mapema juu ya uchaguzi huo.

Nyota wa zamani wa klabu hiyo, Edibily Lunyamila amesema ifikie wakati kuachana na mambo ya kizamani na kupiga kura kwa kujuana, badala yake wachague watakaopeleka mbele.

Lunyimila alisema Yanga inahitaji viongozi ambao hawatakuwa mazoezini kujifunza kuongoza, bali wachaguliwe wenye uzoefu na watakaoivusha salama.

Aliwashauri pia, Wanayanga kuwa makini wakati wa kampeni kuwakwepa viongozi wanaopenda kuahidi vitu vikubwa ilimradi wachaguliwe ilihali wanajua havitekelezeki.

"Ifikie hatua Wanayanga tuepukane na wale wanaotufanya hatuna akili, kwani hata hao ambao wamewahi kuongoza walikuja na sera kibao kwenye makalatasi yao, wengine wakidai watajenga magorofa, wakipata tu uongozi wanataka kunyenyekewa.

"Tunahitaji watu wa kutuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kikubwa ni mabadiliko ya kweli na sio mtu anasema nitafanya hiki mara kile wakati wanakuwa hawana lolote.

"Anayekuja kuongoza Yanga afahamu wazi kwamba kuna watu wenye akili timamu, wapo mawaziri, wabunge, wafanya biashara, wakipato cha chini wenye elimu za juu na wasio na elimu, hivyo sera zao ziwe za kueleweka"alisema.

Jambo lingine aliloliona linatakiwa kuangaliwa kwa umakini zaidi ni kuachana na viongozi ambao wanajirudia rudia pia kujuana kwingi ambako kutafanya wapatikane watu ambao sio sahihi.

"Kwanza lazima Yanga iwe bora kweli kweli kwa maana zinatakiwa kuangaliwa mpaka nafasi za wajumbe wasichaguliwe ili mladi wawekwe watu watakaokuwa na mchango mkubwa na sio kuwepo wepo tu"alisema.

MWANASPOTI

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’