Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwasilisha michango yao ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea
Taarifa ya Yanga iliyotolewa mapema leo imesema Kamati Maalum inayosimamia zoezi la michango haijatoa tathmini rasmi kuhusu zoezi hilo na hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kwa vyombo vya habari
"Kumekua na Taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii zikiwanukuu wajumbe na hata Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa juu ya michango inayoendelea, kiufupi mpaka Sasa Kamati haijawahi kukaa na waandishi ama mwandishi yeyote kutoa tathmini ya michango inayoendelea," imesema taarifa ya Yanga
"Hivyo basi zipuuzieni taarifa ambazo zinasema Kamati imefanikiwa kupata bilioni mbili na kupata wawekezaji"
"Ifahamike kuwa Kazi ya Kamati ni kuratibu na kutafuta fedha kwa ajiri ya Yanga na sio kutafuta wawekezaji Kama ambavyo imekua ikinukuliwa na baadhi ya vyombo vya Habari"
"Sisi kwetu Kamati, mwekezaji ni mwanayanga na mwananchi mwenyewe ndio Maana kauli mbiu yetu katika kuchochea michango ni kuwa Yanga ni timu ya wananchi na wawekezaji ni wananchi mwenyewe"
"Tunathamini michango ya wanayanga kuanzia wanaochanga kiasi kidogo mpaka kikubwa"
"Mpaka Sasa hatujatoa tathmini ya zoezi tunaloendea nalo ,hivyo epukeni uzushi unaofanywa ama kwa makusudi ili kukwamisha juhudi za wanayanga kuchanga ama kwa bahati mbaya"