FT : Njombe Mji 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2017
FT : Njombe Mji 0-1 Yanga
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom, Yanga wamepata ushindi wa kwanza msimu huu baada ya kuifunga Njombe Mji bao 1-0.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Sabasaba mkoani Njombe ulikuwa mkali kwani kila timu ilikuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza msimu huu.

Yanga iliyotawala zaidi kwenye kipindi cha kwanza ilipata bao pekee kwenye dakika ya 15 kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib pembeni kidogo karibu na kibendera cha kona.



Njombe Mji iliyokuwa nyumbani ilitawala zaidi kwenye kipindi cha pili ikijaribu kusaka bao la kusawazisha. Hata hivyo mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand alikuwa kikwazo kikubwa.

Kwenye kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko ambapo Raphael Daudi alichukua nafasi ya Thabani Kamusoko aliyepata majeruhi, Obrey Chirwa aliingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma na Yusuph Mhilu akimbadilisha Emanuel Martini.

Mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo huo.

Yanga iliwakilishwa na;
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Papi Kabamba
7. Juma Mahadhi
8. Thaani Kamusoko/Raphael Daudi
9. Donald Ngoma/Obrey Chirwa
10. Ibrahi Ajib
11. Emanuel Martin/Yusuph Mhilu
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’