Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema Meneja wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro' yuko kwao visiwani Zanzibar anamuuguza mama yake ambaye ni mgonjwa
Kaya amesema Cannavaro aliomba ruhusa kwa uongozi wa timu hiyo na hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa zinazodai kuwa beki huyo wa zamani wa Yanga amefukuzwa
"Cannavaro alifika ofisini na kuomba ruhusa aende kwao akamuuguze mama yake, tulimruhusu," amesema Kaya
"Hizo taarifa zinazodai amefukuzwa hazina ukweli wowote na tunawasihi wanaozusha taarifa hizi waache kwani sio jambo jema kumuharibia mtu ambaye ameitumikia Yanga kwa muda mrefu na kwa heshima kubwa"
Gazeti la Championi toleo la jana lilitoa taarifa hizo zinazodai mkongwe huyo amefukuzwa na kocha Mwinyi Zahera likimtaja bosi wa Simba Mohammed Dewji 'MO' kuwa chanzo cha Zahera kumuondoa Cannavaro.
Hata hivyo gazeti hilo leo limeandika taarifa nyingine likikanusha uhusika wa Mo kwenye sakata hilo


Hivi karibuni uongozi wa Yanga ulilituhumu gazeti la Championi kuwa limekuwa likiandika habari za uongo na upotoshaji zinazoihusu klabu hiyo