Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Yanga dhidi ya Njombe Mji ni matokeo muhimu na yaliyokuwa yanahitajika kwa namna yoyote baada ya sare katika mchezo wa kwanza.
Ni kweli kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa Yanga, kocha Msaidizi Shedrack Nsajigwa alieleza sababu kuwa ni hali ya hewa ya baridi kali.
Nsajigwa amesema Yanga ililazimika kujihami zaidi kwenye kipindi hicho huku ikitumia mashambulizi ya kushitukiza.
Sababu kama hiyo ameitoa nahodha Thabani Kamusoko ambaye alishindwa kumaliza mchezo baada ya kupata maumivu ya misuli.
Baada ya mchezo huo Yanga itasafiri kwenda Songea ambako itashuka tena dimbani Jumamosi Septemba 16 kwenye mchezo mwingine mgumu dhidi ya Majimaji.
Msimu huu utakuwa mgumu sana hasa mikoani, kila timu inaonekana kujipanga vizuri. Ni Mtibwa Sugar pekee iliyoshinda michezo yake yote miwili baada ya mzunguuko wa pili hivyo kukaa kileleni ikiwa na alama sita.
Yanga ina alama nne sawa na Simba, Lipuli na Azam FC.
Ili iweze kutetea ubingwa wake ni lazima Yanga ikusanye alama nyingi kadiri inavyowezekana ugenini huku pia ikihakikisha haipotezi hata alama moja inapocheza kwenye dimba la Uhuru.

ADVERTISE HERE